Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2019

Saratani ya koo la Chakula

Picha
Saratani ya koo ni miongoni mwa magonjwa ya kutisha. Ingawa baadhi ya wagonjwa wa saratani ya koo wanaweza kutibiwa na kupona kabisa, kuna mjadala miongoni mwa matabibu juu ya tiba sahihi ya ugonjwa huu. Bila kujali ni aina gani inayotumika, karibu aina zote za tiba za saratani hii huwa na madhara kwa mgonjwa na wakati mwingine kusababisha kifo badala ya kuponya. Vihatarishi vya kansa ya koo Ingawa chanzo halisi cha kansa ya koo hakijulikani, mambo yafuatayo yanaweza kusababisha mtu kupata saratani ya koo. Hata hivyo, pamoja na kuwepo vihatarishi hivi, ni vigumu kueleza kwa ufasaha kwa nini mtu au watu fulani wanaweza kupatwa na kansa ya koo na mtu mwingine asipate. Vihatarishi hivi ni Umri: Hatari ya kupata saratani ya koo huongezeka zaidi kwa watu walio na umri wa miaka 65 na kuendelea. Hata hivyo saratani ya koo aina ya adenocarcinoma inaweza kutokea hata kwa wanawake walio na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea. Jinsia: Tafiti nyingi zimeonesha kuwa wanaume wana uwezekan...