Machapisho

Saratani ya koo la Chakula

Picha
Saratani ya koo ni miongoni mwa magonjwa ya kutisha. Ingawa baadhi ya wagonjwa wa saratani ya koo wanaweza kutibiwa na kupona kabisa, kuna mjadala miongoni mwa matabibu juu ya tiba sahihi ya ugonjwa huu. Bila kujali ni aina gani inayotumika, karibu aina zote za tiba za saratani hii huwa na madhara kwa mgonjwa na wakati mwingine kusababisha kifo badala ya kuponya. Vihatarishi vya kansa ya koo Ingawa chanzo halisi cha kansa ya koo hakijulikani, mambo yafuatayo yanaweza kusababisha mtu kupata saratani ya koo. Hata hivyo, pamoja na kuwepo vihatarishi hivi, ni vigumu kueleza kwa ufasaha kwa nini mtu au watu fulani wanaweza kupatwa na kansa ya koo na mtu mwingine asipate. Vihatarishi hivi ni Umri: Hatari ya kupata saratani ya koo huongezeka zaidi kwa watu walio na umri wa miaka 65 na kuendelea. Hata hivyo saratani ya koo aina ya adenocarcinoma inaweza kutokea hata kwa wanawake walio na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea. Jinsia: Tafiti nyingi zimeonesha kuwa wanaume wana uwezekan...

Tatizo la ngiri (Hernia)

Picha
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.   Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo. Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni). Dalili za Ngiri Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma. Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na; Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia. U...

Tiba mbadala ya vidonda vya Tumbo

Picha
Dawa za vidonda vya tumbo zinatakiwa zitumike pale panapohitajika tu, siyo maisha yako yote. Kwa kawaida dawa za hospitali mara nyingi huja na maudhi mbalimbali kwa kuwa ni dawa ambazo zimetengenezwa kwa kemikali. Dawa pekee ambazo ni rahisi na za uhakika na hazina madhara ni dawa asili. Changamoto kubwa kwa hapa nchini ni kuwa huduma hii ya tiba asili bado haijapata wataalamu wengi waliobobea wa kutoa bidhaa bora na zenye kufanyiwa utafiti wa kutosha na zenye kiwango cha kimataifa. Vidonda vya tumbo ni nini? Ni kuharibika kwa ukuta wa tumbo la chakula na sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba. Kuna aina kuu mbili za vidonda vya tumbo 1. Gastric ulcers-hivi hutokea kwenye mfuko wa tumbo la chakula. 2. Duodenal ulcers-hivi hutokea sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba. Chanzo cha vidonda vya tumbo ni kuongezeka kwa asidi kwenye tumbo la chakula. Dalili za vidonda Baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo njaa kupita kiasi hasa usiku, tumbo kuwaka moto sehemu ya juu kw...

Homa ya Malale (African Sleeping sickness)

Picha
Ugonjwa wa malale ambao kwa kitaalamu hujulikana kama Human African Trypanosomiasis au African lethargy au sleeping sickness na Congo Trypanosomiasis ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinajulikana kama  Trypanosome .Kuna aina tatu kuu za  Trypanosome  ambazo huathiri binadamu nazo ni; I. Trypanosoma brucei gambiense (T.b.g.) -Hupatikana Afrika magharibi na Afrika ya Kati na husambaa hadi kwenye nchi za Uganda, Kenya na huchangia kwa asilimia 95 ya maambukizi yote ya ugonjwa wa malale.II. Trypanosoma brucei rhodesiense (T.b.r. )-Hupatikana katika nchi za  Afrika Mashariki na zile zilizo kusini mwa bara la Afrika na huchangia asilimia 5 tu ya maambukizi yote ya ugonjwa wa malale III. Trypanosoma cruzi- Hupatikana katika nchi za Amerika ya kati na Amerika kusini na husababisha ugonjwa unaojulikana kama American trypanosomiasis au Chagas disease. Watu 50,000-70,000 wanakisiwa kuambukizwa ugonjwa huu ingawa maambukizi yamepungua katika miaka ya hivi karibuni.Mwaka 20...

Dalili za ugonjwa wa Ebola

Picha
Dalili za ugonjwa wa Ebola ni zipi? Jua dalili za Ebola Dalili za ugonjwa wa Ebola uanza kujitokeza kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi. Mgonjwa wa Ebola huwa na dalili zifuatazo: Homa kali ya ghafla Maumivu ya kichwa Maumivu ya mwili, misuli na viungo Kuharisha (kunaweza kuambatana na damu) Kutapika (kunaweza kuambatana na damu) Vipele mwilini Kuvia damu chini ya ngozi au kutokwa na damu puani, mdomoni, machoni, na masikioni na sehemu ya haja ndogo na kubwa

Ugonjwa wa Kifafa

Picha
UGONJWA WA KIFAFA: CHANZO, DALILI, HUDUMA KWA WAGONJWA NA USHAURI JUU YA MATIBABU Kifafa (Epilepsy) kinatokea kunapokuwa na mapungufu katika seli za ubongo. Ubongo unafanya kazi katika mfumo wa umeme au kama umeme hivi, sasa kunapokuwa na hitilafu katika huu mfumo ndio kifafa kinaweza kutokea ambacho dalili zake ni kuona maluwe luwe (aura), kisha kupoteza fahamu, kuanguka na kutupa miguu na/au mikono, kukaza mdomo, kutoa povu na huwa inamalizia na kutoa haja ndogo au kubwa wakati mwingine. Kifafa sio ugonjwa wa kuambukiza, mara nyingi unakuwa kwenye familia kwa kurithi toka kwa mzazi/wazazi, lakini pia wakati mwingine inaweza tokea baada ya kuumia ubongo kutokana na ajali, kiharusi (stroke), kuumia wakati wa kuzaliwa (birth injuries) etc...Kifafa hiki ni tofauti na 'dege dege' kwa watoto au kifafa cha mimba (Eclampsia). Kifafa hakitibiki, nikiwa na maana hakitibiwi kikapona kabisa...ila kuna dawa za kupunguza au kuzuia kifafa kutokea mara kwa mara. dawa hizi zinapatikan...

Mtoto wa Jicho (Cataract)

Picha
  TATIZO LA MTOTO WA JICHO (CATARACT) Mtoto wa jicho kwa lugha nyingine cataract hutokana na kufanyika kwa ukungu katika lensi ya jicho, mtu aliye na ukungu huu kuona kwake ni sawa sawa na mtu anavyoona nje kupitia dilisha la kioo lenye ukungu wa barafu au maji dilishani mvua inapokuwa inanyesha. Ukungu katika lensi ya jicho husababisha mtu kusindwa kufanya kazi zake kama kuendesha gari, kusoma sana sana usiku au kuona nyuso za watu vyema. Ukungu huu hutokea na kuendeea kufunika jicho zima pole pole kwa muda Fulani na hatimaye mtu anashindwa kuona kabisa. Kwa mara ya kwanza ukungu unapoendelea kutokea mtu anaweza kupata miwani inayoweza kumsaidia kuona lakini baada ya muda Fulani kupita mtu anaweza asione kabisa mpaka afanyiwe matibabu mengine ya upasuaji. Matibabu ya upasuaji ni salama rahisi yenye uhakika na ni ya muda mfupi, huchukua mda mfupi mgonjwa kupona na kurudia kazi zake za kawaida. Jinsi ukungu wa jicho unavyotokea Aina nyingi za ukung...