Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2019

Ugonjwa wa Kifua kikuu (TB)

Picha
Ugonjwa wa kifua kikuu ni kati ya magonjwa matatu yanayotokea sana kwa watu masikini duniani (Disease of poverty). Magonjwa mengine katika jamii ya disease of poverty ni malaria na Ukimwi (AIDS). Ugonjwa wa kifua kikuu huathiri asilimia 98 ya watu katika nchi zinazoendelea, ukimwi asilimia 95 na malaria asilimia 90. Ugonjwa wa kifua kikuu, husababishwa na bakteria wanaojulikana kama Mycobacteria tuberculosis. Kuna aina nyingi za jamii ya Mycobacterium kama Mycobacteria tuberculosis (husababisha kifua kikuu), Mycobacteria leprae (husababisha ugonjwa wa ukoma), Mycobacteria bovis (huathiri ngombe na binadamu), Mycobacteria afrikanum na kadhalika. Ugonjwa wa kifua kikuu unaweza kuathiri mapafu, mishipa ya fahamu, mifupa, mfumo wa mzunguko wa damu, ngozi, viunganishi vya mifupa (joints) na lymphatic system. Kuna aina kuu tatu za ugonjwa wa kifua kikuu Kifua kikuu kinachosababisha madhara (Active tuberculosis) – Hutokea pale ambapo bakteria waliopo mwilini wapo hai na kinga ya mw...

Saratani ya Matiti

Picha
Saratani ni aina ya ugonjwa unaosababisha ukuaji wa seli za mwili kubadilika na kukua bila mpangilio maalum. Saratani ya matiti hutokea kwenye titi ambalo kwa kawaida lina sehemu ya kutengeneza maziwa ijulikanayo kama lobules na aina fulani ya mishipa inayounganisha hizi lobules na chuchu za titi. Sehemu kubwa iliyobakia ya matiti inajumuisha mafuta na tishu ambazo kitaalamu tunazoita connective and lymphatic tissue. Saratani ya matiti inayotokea kwenye lobules huitwa lobular carcinoma na ile inayotokea kwenye ducts huitwa ductal carcinoma. Baadhi ya saratani ya matiti zinaongeza ukubwa kutokana na kuwa na vishikizi aina ya receptors zinazojulikana kama estrogen receptors kwenye seli zao ambazo husababisha ukuaji wa saratani ya matiti. Kuna wanawake wengine wana viashiria vya asili vinajulikana kama HER2 positive breast cancer ambacho husaidia seli kuongezeka, kugawanyika na kujirekebisha pale zinapoharibika. Kiashiria hiki kinaaminika ndicho kinachosababisha wanawake haw...

Upungufu wa Nguvu za kiume

Picha
Katika siku za hivi karibuni kumekua na ongezeka kubwa la upungufu wa nguvu za kiume hasa kwa wanaume waishio maeneo ya mijini. Kwanza tunahitaji kujua kiundani nini maana ya upungufu wa nguvu za kiume chanzo chake pamoja na matibabu yake. Upungufu wa nguvu za kiume kwa ufupi ni Mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa vyema hivyo kupoteza nafasi kubwa ya upatikanaji wa mimba kwa Mwanamke. Tatizo hili limegawanyika katika sehemu kuu 3 1.       Upungufu wa Mbegu za kiume (Low Sperm Count) 2.       Uume kushindwa kusimama Imara (Erectile Dysfunction) 3.       Kushindwa kufikia Mshindo (Prolonged ejaculation)                                                 ...

Anaemia

Picha
Anemia ni hali ya upungufu wa chembechembe ya hemoglobin kwenye seli nyekundu za damu. Hemoglobin ni aina ya protini iliyoundwa na madini ya chuma kwa wingi inayohusika na kusafirisha hewa safi ya oxygen kwenye damu.  Chembechembe hii ndio inayoipa damu wekundu wake. Kumbe basi kwa maelezo haya ni kwamba mtu mwenye Upungufu wa damu (anemia) anapata upungufu wa hewa ya oxgen mwilini kutokana na kwamba vibeba oxygen ni vichache. Pia chembechembe hizi za hemoglobin zinahusika katika kupambana na maradhi, kuganda kwa damu na hizo kuzuia damu kuvuja sana pale mtu anapopata ajali. Upungufu wa madini ya chuma ni chanzo kimojawapo cha kupungukiwa damu mwili kwa mujibu wa taasisi ya kupambana na magonjwa ya Marekani (Center of disease control). Wanawake ni kundi lenye hatari zaidi kupata upungufu huu wa damu kutokana na hedhi. hivo kuna umuhimu wa kuruisha madini ya chuma yanayopotea kwa kula zaidi vyakula vyenye madini ya chuma. Dalili kuu za Upungufu wa Damu Mwilini Pasipo uwepo ...

Ugonjwa wa kipindupindu (Cholera)

Picha
Mojawapo kati ya magonjwa yanayohusishwa na umaskini na uchafu wa kupindukia ni ugonjwa wa Kipindupindu. Inaripotiwa kuwa Kipingupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo huathiri jamii maskini zaidi kwa kiasi kikubwa hasa hasa kwenye nchi zinazoendelea, kiasi kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeuweka ugonjwa huu kama mojawapo ya viashiria vya maendeleo ya jamii husika. Nchini Tanzania hususani katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam, haishangazi basi kusikia kila mwaka kuna mlipuko wa ugonjwa huu pamoja na juhudi kubwa za serikali na mamlaka zake kujitahidi kuhimiza wananchi kupambana na ugonjwa huu. Kipindupindu husababishwa na nini? Ugonjwa huu hutokana na maambukizi katika utumbo mdogo wa binadamu uletwao na vimelea vya bacteria vijulikanavyo kitaalamu kama Vibrio cholerae. Jinsi unavyoweza kuambukizwa Kwa kawaida vimelea hawa hupendelea kuishi katika kinyesi cha binadamu. Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa kunywa maji ama chakula kilichochafuliwa na kinyesi che...

Ugonjwa wa Kiharusi

Picha
Kiharusi ni ugonjwa wa dharura na hatari ambao hutokea pale seli za ubongo zinapokufa kwa kukosa hewa ya oksijeni na chakula kutokana na kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo. Aina za kiharusi Kuna aina kuu mbili za Kiharusi Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo 2. Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo Ukubwa wa tatizo la kiharusi 1. Kiharusi ni muuaji namba 2 : Kwa mwaka 2015 kulingana na ripoti maalumu ya Shirika la Afya duniani WHO kuhusu sababu za vifo ilionesha kiharusi kinashika nafasi ya pili kati ya magonjwa yote kwa kusababisha vifo vingi. 2. Kiharusi husababisha ulemavu kwa wengi : Kiharusi kinashika nafasi ya tatu kati ya visabibishi vya ulemavu duniani. Waathirika wengi huishia kuwa walemavu Dalili za kiharusi 1.GANZI -Mtu anayepata kiharusi hupata ganzi inayoanza ghafla na mara nyingi huathiri upande mmoja wa mwili. Mfano: Upande mmoja wa uso kufa ganzi na kushindwa kuongea vi...

Mawe kwenye kibofu cha mkojo

Picha
Mawe madogo madogo yatokanayo na mgando wa madini ya chumvi hutengenezwa katika kibofu cha mkojo. Wakati mwingine mawe haya husafiri kutoka kwenye figo mpaka kwenye kibofu cha Mkojo. Hali zinazochangia kupata mawe ya kibofu cha mkojo ni pamoja na 1. Kuvimba tezi dume kwa wanaume, 2. Mfumo wa neva kushindwa kufanya kazi vizuri 3. Maambukizi katika njia ya mkojo 4. Kutokunywa maji mengi. Dalili 1. Mauvivu wakati wa kukojoa                                                                                                                                                               ...