Homa ya Malale (African Sleeping sickness)

Ugonjwa wa malale ambao kwa kitaalamu hujulikana kama Human African Trypanosomiasis au African lethargy au sleeping sickness na Congo Trypanosomiasis ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinajulikana kama Trypanosome.Kuna aina tatu kuu za Trypanosome ambazo huathiri binadamu nazo ni;

I.Trypanosoma brucei gambiense (T.b.g.)-Hupatikana Afrika magharibi na Afrika ya Kati na husambaa hadi kwenye nchi za Uganda, Kenya na huchangia kwa asilimia 95 ya maambukizi yote ya ugonjwa wa malale.II.Trypanosoma brucei rhodesiense (T.b.r.)-Hupatikana katika nchi za 

Afrika Mashariki na zile zilizo kusini mwa bara la Afrika na huchangia asilimia 5 tu ya maambukizi yote ya ugonjwa wa malale

III.Trypanosoma cruzi-Hupatikana katika nchi za Amerika ya kati na Amerika kusini na husababisha ugonjwa unaojulikana kama American trypanosomiasis au Chagas disease.

Watu 50,000-70,000 wanakisiwa kuambukizwa ugonjwa huu ingawa maambukizi yamepungua katika miaka ya hivi karibuni.Mwaka 2009, maambukizi yalikuwa 10,000 ambapo katika taarifa ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ya Januari mwaka 2012, limesema, maambukizi haya chini ya elfu kumi ni ya kwanza kuripotiwa katika kipindi cha miaka 50 iliyopita. Maambukizi 7,319 yaliripotiwa mwaka 2010.Ugonjwa huu wa malale umeua watu 48,000 mwaka 2008.



Dalili na viashiria vya ugonjwa wa malale


Dalili ya kwanza ni maumivu makali yanayotokana na kungatwa na mdudu aina ya Mbungo. Sehemu ambayo imengatwa na Mbungo huwa nyekundu (inflamed) na kama mtu atakuwa amepata maambukizi ya ugonjwa wa malale baada ya kungatwa na Mbungo basi maumivu hujirudia tena baada ya siku 10 na sehemu ile huvimba (‘trypanosomal chancre’) na tezi zilizokaribu na sehemu hiyo iliyongatwa huvimba (‘Winterbottom sign’).


Ndani ya wiki 2-3, vimelea vya trypanosomehuingia kwenye mfumo wa damu.

Dalili za ugonjwa huu hutokea kwa awamu mbili;

Awamu ya kwanza hujulikana kama haemolymphatic phase na huambatana na homa kali, maumivu ya mifupa,kichwa kuuma na kuwashwa mwili. Kuathirika kwa mfumo wa lymph (lymphatic system) na wa damu huambatana na kuvimba sana kwa tezi. Kuvimba kwa tezi nyuma ya shingo hutokea (‘winterbottom sign’) na kama mgonjwa hatapata tiba, kinga ya mwili huzidiwa nguvu na ugonjwa huu na hivyo kusababisha kuathirika kwa figo, moyo (myocarditis), mapafu kujaa maji, (pleural effusion), ugonjwa wa ini (hepatitis),upungufu wa damu mwilini (anemia),na kuathirika kwa mfumo wa homoni (endocrine system).


•Awamu ya pili inayojulikana kama neurological phase, hutokana na kuathirika kwa mfumo wa fahamu kutokana na vimelea vya ugonjwa wa malale kuwa na uwezo wa kuvuka kinga ya ubongo (blood brain barrier) ambapo ndio jina la ugonjwa wa malale (sleeping sickness) linapopatikana kwani mgonjwa huwa na dalili za mtu kuchanganyikiwa, kuharibika kwa utaratibu wa kulala (mtu kutopata usingizi usiku na 

kulala wakati wa mchana), uchovu. Iwapo mgonjwa hatapata tiba wakati huu, basi mgonjwa huweza kupata ugonjwa wa akili pamoja na kupoteza fahamu au kuingia kwenye koma (coma). Kuathirika kwa mfumo wa fahamu hakuwezi kurekebishika na mgonjwa hudumu na hali hiyo kwa kipindi chote cha maisha yake yote. Hali ya kuhisi usingizi kila wakati hutokana na kemikali aina ya Tryptophol inayotolewa na vimelea vya ugonjwa wa malale.


Maambukizi ya Trypanosome brucei rhodesiense huwa ya ghafla na hatari sana kuliko ya Trypanosome brucei gambiense na mgonjwa huweza kufariki kabla hajaingia kwenye awamu ya pili (‘neurological phase’).Iwapo maambukizi haya ya Trypanosome brucei rhodesiense sio makali, 

mgonjwa huingia kwenye awamu ya pili ya neurological phase na hatimaye hupoteza fahamu au huingia kwenye koma (coma).

Maambukizi ya Trypanosome brucei gambiense, huwa sio makali kwani yanaweza kutokea taratibu kwa muda wa mwezi au baada ya miaka mingi, ambapo mgonjwa atakuwa anapata homa za mara kwa mara,kuvimba ini na bandama (spleen), kuvimba tezi ambazo huwa ngumu,ndogo (discrete),zinazoteleza (rubbery), zisizokuwa na maumivu. Ikiwa mgonjwa hatapata tiba,baada ya miezi kadhaa mgonjwa ataingia kwenye awamu ya pili ya neurological phase.


Tiba ya ugonjwa wa malale


Tiba ya ugonjwa huu hutolewa bure kulingana na hatua ya ugonjwa wa malale.

Mgonjwa aliye kwenye hatua ya kwanza (Haemolymphatic phase) hutibiwa kwa dawa aina ya Pentamidin au Suramin. Dawa hizi hazina madhara sana na ni rahisi kutumiwa.

Mgonjwa aliye kwenye hatua ya pili (Neurological phase) hutibiwa kwa kutumia Melarsoprol, Eflornithine (ambayo ni ya uhakika dhidhi ya Trypanosome brucei gambiense tu), pamoja na tiba ya mchanganyiko wa nifurtimox na eflornithine.Dawa hizi zina madhara na matumizi yake 

yanahitaji uangalifu mkubwa na umakini. Melarsoprol husababisha madhara ya ubongo yajulikanayo kama reactive encephalopathy (encephalophatic syndrome) ambayo huweza kusababisha kifo kwa asilimia 3-10.

Bila tiba, mgonjwa wa ugonjwa wa malale huweza kufariki ndani ya miezi sita kutokana na kuathirika moyo (cardiac failure) au kutokana na maambukizi ya Trypanosome brucei rhodesiense yenyewe.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Saratani ya koo la Chakula

Tiba mbadala ya vidonda vya Tumbo