Ugonjwa wa Kifafa
UGONJWA WA KIFAFA: CHANZO, DALILI, HUDUMA KWA WAGONJWA NA USHAURI JUU YA MATIBABU
Kifafa (Epilepsy) kinatokea kunapokuwa na mapungufu katika seli za ubongo. Ubongo unafanya kazi katika mfumo wa umeme au kama umeme hivi, sasa kunapokuwa na hitilafu katika huu mfumo ndio kifafa kinaweza kutokea ambacho dalili zake ni kuona maluwe luwe (aura), kisha kupoteza fahamu, kuanguka na kutupa miguu na/au mikono, kukaza mdomo, kutoa povu na huwa inamalizia na kutoa haja ndogo au kubwa wakati mwingine.
Kifafa sio ugonjwa wa kuambukiza, mara nyingi unakuwa kwenye familia kwa kurithi toka kwa mzazi/wazazi, lakini pia wakati mwingine inaweza tokea baada ya kuumia ubongo kutokana na ajali, kiharusi (stroke), kuumia wakati wa kuzaliwa (birth injuries) etc...Kifafa hiki ni tofauti na 'dege dege' kwa watoto au kifafa cha mimba (Eclampsia).
Kifafa hakitibiki, nikiwa na maana hakitibiwi kikapona kabisa...ila kuna dawa za kupunguza au kuzuia kifafa kutokea mara kwa mara. dawa hizi zinapatikana hospitali, na mgonjwa atakunywa kwa maisha yake yote dozi inategemea na hali ya mgonjwa anapoonwa mara kwa mara kwenye kliniki zao maalum. Kwa sababu kifafa hutokea ghafla, ni muhimu sana mgonjwa anapoanguka utoe vitu vyote vya hatari vyenye kuumiza (watu wengi hukimbilia kumtoa mgonjwa au kumshika na pengine hata kumfunga kamba...hii si sahihi, inatakiwa utoe vitu vitakavyohatarisha mgonjwa kuumia au hata kufa) mfano moto, jiko, vifaa vyenye ncha kali etc. Kuna wagonjwa wengine huwa wanashtukia kifafa kinapoanza (aura) hivyo kujiepusha na sehemu za hatari.
Baada ya kuanguka kifafa, mgonjwa anaweza akawa kama hana fahamu sawa sawa, amechanganyikiwa au hata kama kichaa...mara nyingi anahitaji msaada badala ya kumnyanyapaa. Siwezi kukushauri umtimue au usimtimue housegirl wako sababu sijui kwa nini wataka kufanya hivyo...kama unaogopa kuwa atawaambukiza, si kweli...kifafa hakiambukizi, kama unaogopa majukumu ya kumlea mgonjwa wa kifafa...lakini kama una moyo wa kumsadia, mpeleke Muhimbili pale Idara ya magonjwa ya akili kuna wataalamu waliobobea, na kuna kliniki maalum kwa ajili ya wagonjwa wa kifafa atapata msaada unaostahiki na maisha yake yataboreka kadri amabavyo zile attacks za kifafa zinapungua.

Maoni
Chapisha Maoni