Anaemia
Anemia ni hali ya upungufu wa chembechembe ya hemoglobin kwenye seli nyekundu za damu. Hemoglobin ni aina ya protini iliyoundwa na madini ya chuma kwa wingi inayohusika na kusafirisha hewa safi ya oxygen kwenye damu. Chembechembe hii ndio inayoipa damu wekundu wake. Kumbe basi kwa maelezo haya ni kwamba mtu mwenye Upungufu wa damu (anemia) anapata upungufu wa hewa ya oxgen mwilini kutokana na kwamba vibeba oxygen ni vichache. Pia chembechembe hizi za hemoglobin zinahusika katika kupambana na maradhi, kuganda kwa damu na hizo kuzuia damu kuvuja sana pale mtu anapopata ajali.
Upungufu wa madini ya chuma ni chanzo kimojawapo cha kupungukiwa damu mwili kwa mujibu wa taasisi ya kupambana na magonjwa ya Marekani (Center of disease control). Wanawake ni kundi lenye hatari zaidi kupata upungufu huu wa damu kutokana na hedhi. hivo kuna umuhimu wa kuruisha madini ya chuma yanayopotea kwa kula zaidi vyakula vyenye madini ya chuma.
Dalili kuu za Upungufu wa Damu Mwilini
Pasipo uwepo wa vibeba oksijeni kwenye damu, maeneo mbalimbali ya mwili yatakosa hewa na kupeleka ufanisi kupungua, sehemu hizi ni misuli, viungo kama moyo na ubongo, tishu mbalimbali na seli za mwili. Dalili kuu ni kuhisi umechoka na mwili kutokuwa sawa muda mwingi. Zifuatazo ni dalili za upungufu wa damu (anemia)
- Mwili kukosa nguvu na uchovu wa mara kwa mara
- Mapigo ya moyo kubadilika badilika na moyo kwenda mbio sana
- Kupumua kwa shida na stamina kupungua
- Maumivu ya kifua
- Kusinzia sana na mwili kutokuwa sawa
- Mikono kuwa ya baridi na
- Kupata maumivu ya kichwa
Muhimu kufahamu ni kwamba anemia huanza taratibu bila kuonesha dalili zozote lakini tatizo huwa linazidi kuwa kubwa kadiri muda unavoenda na hasa pale ikiwa kuna vitu hatarishi zaidi ya kimoja vinavyopelekea anemia.
Kuna sababu kuu tatu za kwanini umepata anemia (upungufu wa seli nyekundu za damu) ambazo ni mwili kutotengeneza seli nyekundu za kutosha, kupoteza damu nyingi kwenye ajali na mwili wenyewe kupambana na seli nyekundu za damu. Hapa chini ni mazingira na vihatarishi vinavyopelekea anemia
- Upungufu wa madini ya chuma au Vitamin B12. Hii inaweza kukutokea endapo unaaacha kula baadhi ya chakula, au kwa watu wasiokula kabisa nyama na mazao ya wanyama. Mwili unahitaji zaidi madini ya chuma na Vitamin B12 ili kutengeneza chembechembe za hemoglobin.
- Wanawake wapo kwenye hatari zaidi ya kupata upungufu wa damu kuliko wanaume kutokanana kupoteza damu nyingi kipindi cha hedhi.
- Wazee na wenye umri mkubwa. Tafiti zinasema kwamba watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wapo kweye hatari zaidi ya kupata upungufu wa damu.
- Wajawazito
- Ukuaji wa fangasi wa candidakupita kiasi hupunguza uwepo wa mwili kufyonza Vitamins.
- Magonjwa ya autoimmune ambapo kinga ya mwili inashambulia seli za mwili, saratani, Ukimwi na Figo
- Matatizo kwenye mfumo wa chakula yanayopelekea uchakataji wa chakula kuvurugika na mwili kushindwa kuvyonza madini na vitamin za kutosha.
- Kumeza vidonge mara kwa mara mfano vidonge vya kupunguza maumivu hasa asprin.

Maoni
Chapisha Maoni