Homa ya Dengue

Homa ya Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi wanaosambazwa na mbu wakati wa mchana. Virusi hawa wana uhusiano wa karibu na virusi wanaosababisha homa ya manjano.


Dalili ya Homa ya Dengue
1. Homa kali ya ghafla.
2. Kichwa kuuma sana
3. Maumivu nyuma ya macho
4. Maumivu kwenye viungo na misuli
5. Mwili kupoteza nguvu
6. Kichefuchefu na kutapika
7. Kutokwa na damu kwenye fizi na pua


Matibabu
Hakuna matibabu rasmi ya kutibu ugonjwa wa Dengue. Unapoona dalili za dengue tumia dawa za kutuliza maumivu jamii ya Paracetamol / Panadol.
Usitumie Asprin ni mbaya kwa ugonjwa huu.


Jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu.
1. Jikinge na mbu hasa wakati wa mchana.
2. Tumia dawa za kufukuza mbu
3. Vaa nguo ndefu za kuziba sehemu za mikono na miguu.
4. Angamiza mazalia ya Mbu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Saratani ya koo la Chakula

Tiba mbadala ya vidonda vya Tumbo

Homa ya Malale (African Sleeping sickness)