Ugonjwa wa Kaswende (Syphilis)
Kaswende ni mojawapo kati ya maradhi ya zinaa, ambapo husababishwa na bacteria anayefahamika kama Treponema Pallidum.
Dalili za kaswende zimegawanyika katika makundi manne (4) kulingana na hatua ya ugonjwa.
Hatua ya Kwanza.
1. Kutokwa na vidonda sehemu za siri.
2. Tezi kuvimba karibu na sehemu iliyo na kidonda.
Hatua ya Pili.
1. Uchovu
2. Kuumwa Kichwa
3. Homa.
4. Nywele kunyofoka.
5. Vidonda vya koo.
6. Kuvimba matezi.
7. Maumivu ya mifupa.
Hatua ya Tatu.
Hatua hii ugonjwa hujificha na kutoonesha dalili zozote na hapa mgonjwa hujihisi amepona bila kufanya matibabu yoyote.
Hatua ya Nne.
1. Upofu
2. Magonjwa ya moyo.
3. Mtu kuwa kiziwi.
4. Kupungukiwa kumbukumbu.
5. Kifo.
Jinsi ya Kujikinga.
1. Ngono salama tumia condom
2. Acha ngono kabisa
3. wajawazito kuhudhuria clinic mapema.

Maoni
Chapisha Maoni