Ugonjwa wa kipindupindu (Cholera)
Mojawapo kati ya magonjwa yanayohusishwa na umaskini na uchafu wa kupindukia ni ugonjwa wa Kipindupindu. Inaripotiwa kuwa Kipingupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo huathiri jamii maskini zaidi kwa kiasi kikubwa hasa hasa kwenye nchi zinazoendelea, kiasi kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeuweka ugonjwa huu kama mojawapo ya viashiria vya maendeleo ya jamii husika. Nchini Tanzania hususani katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam, haishangazi basi kusikia kila mwaka kuna mlipuko wa ugonjwa huu pamoja na juhudi kubwa za serikali na mamlaka zake kujitahidi kuhimiza wananchi kupambana na ugonjwa huu.
Kipindupindu husababishwa na nini?
Ugonjwa huu hutokana na maambukizi katika utumbo mdogo wa binadamu uletwao na vimelea vya bacteria vijulikanavyo kitaalamu kama Vibrio cholerae.
Jinsi unavyoweza kuambukizwa
Kwa kawaida vimelea hawa hupendelea kuishi katika kinyesi cha binadamu. Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa kunywa maji ama chakula kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea hivi vya kipindupindu.
Dalili za kipindupindu ni zipi?
Dalili za mwanzo kabisa za kipindupindu ni
• Kuanza Kuharisha ghafla choo chenye majimaji (ambacho rangi yake ni kama maji ya mchele) na chenye harufu mbaya kama shombo ya samaki.
• Kutapika
• Kuanza Kuharisha ghafla choo chenye majimaji (ambacho rangi yake ni kama maji ya mchele) na chenye harufu mbaya kama shombo ya samaki.
• Kutapika

Aidha mgonjwa wa kipindupindu huonesha dalili zakupungukiwa maji mwilini kama vile
• ngozi huwa kavu,
• midomo kukauka,
• mgonjwa kuhisi kiu kikali,
• machozi kutoweza kutoka,
• kupata mkojo kidogo sana,
• Kuishiwa nguvu na kujisikia mchovu sana.
• Macho kutumbukia ndani hasa kwa watoto.
• ngozi huwa kavu,
• midomo kukauka,
• mgonjwa kuhisi kiu kikali,
• machozi kutoweza kutoka,
• kupata mkojo kidogo sana,
• Kuishiwa nguvu na kujisikia mchovu sana.
• Macho kutumbukia ndani hasa kwa watoto.
Jinsi ya kuzuia kipindupindu
Mara kwa mara serikali na taasisi zake zimekuwa zikihimiza watu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu wa kupindupindu. Miongoni mwa njia zinazofaa katika kuzuia milipuko ya ugonjwa huu ni
- Upatikanaji wa maji safi na salama, watu hawana budi kuhakikisha kuwa maji ya kunywa yanachemshwa vyema kabla ya kuyanywa. Vile vile wanaweza kutumia chlorine katika maji ambayo huua vimelea hawa wa V. cholerae.
- Ni muhimu kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula
- Tunashauriwa kufunika chakula kikiwa mezani ili nzi wasitue juu yake
- Inashauriwa kujenga choo umbali wa angalau mita 30 kutoka chanzo cha maji
- Inashauriwa kwa wasafiri watokao nchi zilizoendelea kupata chanjo iitwayo Dukoral, pindi wanaposafiri kwenda nchi zinazoendelea.

Maoni
Chapisha Maoni