Ugonjwa wa U.T.I


Urinary Tract Infection (U.T.I) ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria anaoshambulia wanawake zaidi katika mfumo wa haja ndogo. Ugonjwa huu hushambulia sehemu za kibofu cha mkojo, mirija ya mkojo (urethra) na wakati wa hatua mbaya hufika kwenye figo kama hautafanyiwa matibabu.


Dalili za ugonjwa
1. Maumivu makali wakati wa haja ndogo.
2. Kukojoa mara kwa mara kiasi kidogo cha mkojo.
3. Maumivu sehemu za nyonga na tumbo.
4. Uchovu


Matibabu
1. Tumia dawa za anti-biotics kwa ugonjwa usio wa kujirudia.
2. Kwa ugonjwa wa kujirudia muone daktari kwa vipimo zaidi.


Jinsi ya kujikinga
1. Kunya maji mengi
2. Oga na maji mengi ya kutiririka (shower)
3. Osha sehemu za siri kwa maji safi.
4. Hakikisha sehemu za siri zinakua kavu muda wote.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Saratani ya koo la Chakula

Tiba mbadala ya vidonda vya Tumbo

Homa ya Malale (African Sleeping sickness)