Upungufu wa Nguvu za kiume
Katika siku za hivi karibuni kumekua na ongezeka kubwa
la upungufu wa nguvu za kiume hasa kwa wanaume waishio maeneo ya mijini. Kwanza
tunahitaji kujua kiundani nini maana ya upungufu wa nguvu za kiume chanzo chake
pamoja na matibabu yake.
Upungufu wa nguvu za kiume kwa ufupi ni Mwanaume
kushindwa kufanya tendo la ndoa vyema hivyo kupoteza nafasi kubwa ya
upatikanaji wa mimba kwa Mwanamke.
Tatizo
hili limegawanyika katika sehemu kuu 3
1. Upungufu
wa Mbegu za kiume (Low Sperm Count)
2. Uume
kushindwa kusimama Imara (Erectile Dysfunction)
3. Kushindwa
kufikia Mshindo (Prolonged ejaculation)
Upunguvu
wa mbegu za kiume (Low Sperm Count)
Kwa kawaida wakati wa kufanya tendo la ndoa mwanaume
hutoa shahawa (mchanganyiko wa mbegu za uzazi na simeni). Shahawa huwa na rangi
ya maziwa iliyokoloea. Kwa mwanaume mwenye tatizo la nguvu za kiume hutoa
shahawa zilizo na rangi ya maziwa za kufifia na wengine hutoa shahawa zenye
rangi ya maji kabisa.
Jinsi ya kutibu aina hii ya tatizo
1. Fanya
mazoezi mara kwa mara ili kuongeza kiasi cha homoni za testosterone
2. Kula
vyakula vya kuongeza vitamin C kama matunda.
3. Punguza
au acha matumizi ya Pombe
Uume
kushindwa kusimama (Erectile Dysfunction)
Mambo yanayochangia uume kushindwa kusimama ni pamoja
na matumizi ya vyakula vyenye mafuta mengi, uzito uliopita kiasi, matatizo ya
kisaikolojia (stress) na matumizi ya Soya na Pombe kali. Njia nzuri ya
kupambana na aina hii ni kujua chanzo ni nini na kukiepuka.
Kushindwa
kufikia mshindo (Prolonged Ejaculation)
Katika hali hii mwanaume hutumia muda mrefu sana kutoa
shahawa na wakati mwingine shahawa hushindwa kutoka kabisa. Aina hii
visababishi vyake hufanana na vile vya uume kushindwa kusimama.

Maoni
Chapisha Maoni